Monday, April 23, 2007

Nimekutana na mwanaharakati, Faustine Munishi!


Ililikuwa ni siku njema sana kwangu, nimekutana na mwanaharakati ambaye baadhi ya watanzania, wakiwemo viongozi wa dini wanamuona kama hamnazo, kana kwamba amrukwa na akili. Ni miongoni mwa watu ambao niliomba nisife bila kuwaona! Inawezekana kweli huyu ndugu amekuwa kichaa, lakini pia naona kama vile kichaa chake kina nafuu kubwa, kina faida, kichaa chake kimempelekea kuwa mwana harakati wa demokrasia na utawala bora Tanzania.

Huyu ndugu anataka kugombea urais wa Tanzania siku za usoni, hili nalo limekuwa kero kwa baadi ya watanzania wenye wivu na akili fupi na wavivu wa kufikiri. Nasema hizvyo kwa sababu katiba ya Tanzania inamruhusu mtu yeyote mwenye sifa zilizoainishwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi Tanzania, kulikoni leo huyu jamaa akitangaza kugombea aonekane mhaini?

Namzungumzia Faustin Munishi, mwimbaji maarufu na mkongwe wa nyimbo za injili Tanzania, ambaye nilikutana naye kwa mara ya pili jijini Nairobi Ijumaa ya tarehe 19/04/2007, mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2005. Ni mwimbaji anayetunga nyimbo zenye ujumbe unaogusa rika zote, sasa amegeuka anaimba nyimbo za kuhamasisha mapibadiliko katika nchi yetu. Kuna watu wakiwemo viongozi wa dini Tanzania wamekuja juu na kumshutumu Munishi kwa kuchanganya siasa na dini.

Nilipata shida sana kwa watu hawa kumshutumu Munishi kwa kufanya hivyo, sio mara yao ya kwanza kufanya hivyo, miaka ya karibuni waliwahi kumshutu Askofu mkuu wa Kanisa la Full Gozpel Bible Fellowship, Zakaria Kaobe kwa kuikosoa CCM hadharani. Wakasahau kuwa Kakobe ni Mtanzania, ana haki ya kusema kwa mujibu wa katika Kifungu 18(a). Tofauti ya Mkapa na Kakobe ni kwamba, Mkapa alikuwa rais, wakati Kakobe ni Askofu, lakini wote ni Watanzania. Wana haki sawa kikatiba.


Munishi ameinuka, sio leo, kaanza muda, lakini kwa mujibu wa moja ya makala zake katika tovuti yake, anasema wakati ule kulikuwa hakuna uhuru wa kutosha wa vyombo vya habari nchi, angesemea wapi? Munishi anadai mabadiliko nchini, hii ni haki ya watanzania wote, bila kujali dini zao, itikadi zao na makabila yao, mabadiliko yanapobidi, basi ni haki yao.

Munishi anawaelezea wachungaji wanaomshutumu kwa kuchanganya siasa na dini kuwa hata wao wanashiriki siasa, pengine kwa kutokujua. Wakati wanapo wahimiza waumini wao kwenda kupiga kura wanashiriki siasa, wanapoalikwa kwenye hafla za kuapisha raois na wao kukubali mialiko hiyo, tayari wameshiriki siasa.

Kwa ufupi nimejisikia vizuri kuwa na mwanaharakati huyu, Faustin Munishi, mwana wa Tanzania, mpenda demokrasia na asiyekata tamaa.