Wednesday, March 21, 2007

SALAMU

Hivi karibuni nimepata taarifa kwamba serikali inapitisha wimbo utakaotuika kama wimbo wa taifa la Shirikisho la Afrika Mashariki. Je wewe una habari hiyo? Umekwisha jiuliza kwa nini wameamua kuutafuta wimbo huo? In maana kwamba wameshapitisha maamuzi ya kuiingiza Tanzania katika shirikisho, tatizo langu sio shirikisho, tatizo ni kwamba je wananchi wamekubali kujiunga.

Kama Wananchi hawajakubali na bado serikali ikapitisha, huu si ubabe? Ngoja kwanza niendelee kufanya utafiti, nitakuandalia makala kamili, usiache kumtaarifu Issa Michuzi, Maggid Mjengwa, Boniface Makene na Ndesanjo Macha.