Tuesday, May 29, 2007

Eti daladala zinakatisha ruti, mnamwambia nani maneno hayo?


Nasikia tunailalamikia serikali kuwa daladala zinakatisha ruti, eti kwamba hazifiki kule zilikopangiwa kufika ba hivyo kusababisha usumbufu kwa abiria. nataka nijue, wakati wanakatisha hizo ruti ninyi abiria mnakuwa wapi?
nauliza hivi si kwa nia ya kuwatetea watu wa daladala, isipokuwa nimegundua kuwa baadhi usumbufu mwingi tunaoupata wananchi wa Tanzania husababishwa na sisi wenyewe. Naongea hivi nikimaanisha sambamba na uchungu nilionao.
Hivi karibuni nilikuwa nasafiri kuelekea Tanga, gari (basi) tulilokuwa tumepanda lilijaza kiasi cha abiria wengine kusimama. Tulipofika kituo cha Kibaha, askari mmoja wa usalama barabarani alisimamisha lile gari na kulitaka kutoendelea na safari
Ndugu yangu kilichotokea kilinishangaza, abiria wakawa wanampinga yule trafiki kwa kitendo chake cha kuwashusha abiria waliozidi kinyume na sheria za usalama barabarani. Wakati huo siku chache zilizopita nilikuwa nimetoka kuzungmza na maofisa wa Wizara ya miundo mbinu kuhusu suala la abiria kupunguzwa na kukalia vigoda kwenye baadhi ya mabasi ya mikoani.

Friday, May 25, 2007

HUU MCHEZO UFE MARA MOJA!!!



Ni kama vile nasema "ole wenu ninyi waandishi, mnaonunuliwa na wakubwa na kuikosesha jamii ya watanzania haki ya kuhabarishwa! hakuna, kataeni, muwe na huruma na jamii ambayo inawategemea kuwasemea kule ambako wao hawawezi kusema!

Ni haki yetu kusema, kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania 18(a)

Thursday, May 24, 2007

NDESANJO MACHA TUSAIDIE!

Ndesanjo unisamehe buree, nimeitumia picha yako hapa! Naona uko na mheshimiwa Michuzi!


Salaam kwa wanablogu za kiswahili wowote na popote mlipo!
Pengine salaam hizi ni maalum zaidi kwa Ndesanjo Macha kule USA! Huyu ndiye aliyenichochoea na kunielimisha kupitia makala zake katika gazeti la Mwananchi jumapili. Naam, nilitoka jasho kwelikweli, nilidhani ni kazi kweli kufungua blogu, mpaka nikafikia hatua ya kumuomba Ndesanjo anifungulie mwenyewe!


Hatimaye! Nasema hatimaye nimefungua blogu yangu sasa, uwanja wa kusemea yale yaliyo mawazo yangu, sasa ombi langu ni kwako Ndesanjo, naomba unisaidie namna ambavyo nitajiunga na ule umoja wa wana blogu za kiswahili! Kila la heri na YESU ANAKUPENDA!

Wednesday, May 23, 2007

Na sisi tunazo jamani!





Kuna watu wanafikiri mimi Mkenya kwa kuifagilia Windsor, jamani penye ukweli si tunapaswa kusimama? Hizo hapo juu ni baadhi ya Hoteli zetu nzuri hapa Zipo zingine kule Zanzibar. Kwa leo nimekutafutia hizi.
Ya kwanza kule juu ni Movenpick Hotel, iko mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam, imeshabadilishwa majina mara kibao, inadaiwa kuwa wanakwepa kodi, mabepari (wawekezaji) ndio wamiliki tofauti na ile ya Kenya. Ingine ni Kilimanjaro Kempisk, zamani iliitwa Kilamnjaro Hotel, nashukuru tu, katika kukarabati kwao (maana hukarabati mpaka majina) jina la mlima wetu limebaki. Kwa mujibu wa mtandao Hoteli zote hizi mbili zina hadhi ya nyota tano! 5* star

Tuesday, May 22, 2007

WINDSOR GOLF HOTEL & COUNTRY HOTEL








Watu kama sisi tulilala vyumba kama hivi, nafikiria kufanyia 'Honey Moon' yangu hapa!




Jengo hili la kwanza ndio kila kitu, mapokezi, sehemu ya chakula na vinginevyo, lakini yale majengo yanayofuatia ni vyumba vya kulala wageni


Hii ndio Windsor unavyoweza kuina kwa juu, nyuma kuleeee, ni jiji la Nairobi



Hii ni Hotel ambayo tulifikia tukiwa jijini Nairobi, sio siri nili 'enjoy' kwelikweli, siku moja nitakupa stor kuhusu Hoeli hii. lakini moja ya mambo yaliyonifurahisha ni kwamba, ni Hoteli kubwa ya kimataifa, yenye hadhi ya nyota tano 5* Hotel inayomilikiwa na Mkenya tena ameajiri wazungu katika Hoteli hiyo.




Monday, May 21, 2007

Nyerere analia au anacheka?
Najaribu kuwaza ikiwa watu wangekuwa wanakufana na kisha kupewa nafasi ya kurudi duniani, naamini pengine Nyerere angelia, si kuja duniani tu, hata ingekuwa kwamba wafu wangekuwa wanaruhisiwa kupokea taarifa mbalimbali kutoka duniani, tabasamu hili la hayati Nyerere lisingeonekana! Angekuwa analia! sababu unazijua!

MATUMIZI YA PESA ZA UMMA!

Ni muhimu mara nyingine kukaa pamoja na kujadili masuala mbambali yanayohusu taifa letu. Hii ni moja ya mijadala ya wanafunzi kuhusu matumizi ya pesa za wananchi. hapo niliigiza kama waziri wa habari, utamaduni na michezo. Chuo kikuu cha Tumaini Iringa. Kushoto ni Jozaka na yule binti pale anaitwa Caroline na yule mwenye upara ni Balikudembe