Wednesday, April 25, 2007

Kikwete ana maswali ya kuwajibu watanzania!

Rais Kikwete, akiwa na waziri mkuu wa Italy, bwana Romano Prodi




Ana mwaka na meiezi tangu achaguliwe kuwa rais wa Tanzania, sikuwepo wakati wa Nyerere, na nilikuwa mdogo sana wakati wa Mwinyi, lakini siamini wala kudhani kuwa kuna rais aliyewahi kuchaguliwa klwa kishidndo kama Kikwete, ikiwa CCM hawakuiba kura.

Wakati wa kampeni aliwaahidi mwakubwa watanzania, alisema CCm itawawezesha wanawake, alitamba kuleta maisha bora kwa kila mtanzania. Na alisisitiza hivyo hata baada ya kuapishwa. Wakati anaahidi hivyo kuna watu wakiwemo wanasiasa walimuonea huruma badala ya kumpongeza, walimshangaa! Kamwe usinilulize kwa nini walimshanga na kumuonea huruma. Naweza kukisia tu kwamba, kwa mfano, kitendo cha kuahidi ajira milioni moja kwa watanzania kilipelekea baadhi ya watu kumsikitikia, pengine walijua kuwa wazo la kuwapa ajira milioni moja watanzani ni kama ndoto na kuwarubuni watanzania. Nasema hivi, nadhani hivyo!

Kikete hakuacha majigambo, alipoingia madarakani aliendeleza hali hiyo, ni pale alipotaka kuuonyesha ulimwengu kuwa amedhamiria kupambana na rushwa na kutokomeza kabisa dawa za kulevya. Akavuka mipaka mtoto wa Mrisho, akasma eti wala rushwa anawajua na wauzaji wa dawa za kulevya anawajua, ila anawapa muda wa kujirekebisha. Hebu fikiria, mtu alidhulumu haki za watu kwa miaka nenda rudi, kwa kununua na kuuza haki za watanzania, eti anapewa muda wa kujirekebisha, kana kwamba alikuwa hajui kuwa napaswa kujirekebisha. Mtu aliyeharibu maisha ya vijana wengi wa Tanzania, walioacha masomo kwa sababu ya kuathiriwa na dawa za kulevya, eti anapewa muda wa kujirekebisha. Kwa leo sio hoja yetu hiyo.

Kikwete alishatamba kwa kusema hayo aliyokwisha yasema, lakini maswali ya watanzania tuliowengi ni kwamba, kilichomfanya awpe muda wahalifu hao ni nini hasa, kwa nini awape muda, ndio swali la wengi nchini.

Anasema anawajua, anazungumza hivyo akijua kuwa yeye ni nani, nina maana kwamba yeye ni rais, aliyeapa kutochekelea rushwa, ni kikwete huyo huyo aliywatahadharisha wabunge alipokuwa akiwahutubia kwa mara ya kwanza kuwa wasje wakadanganywa na tabasamu lake! Mheshimiwa rais, watu wanauliza kwa nini umewahifadhi wala rushwa, kuna ajenda gani ya siri? Kwa nini umewahifadhi wale wanajihusisha na dawa za kulevya? Huoni kwamba kuwapa kwako muda wa kujirekebisha ni kuwapa muda wa kufanya biashara zaidi, kula rushwa zaidi, ili watakapotoka wawe wamekisanya faida ya kuanzia biashara zingine halali? Watanzania wangapi watakuwa wameathirika na kupewa muda kwa hawa jamaa?

Fikiria ikiwa uliyempa muda ni hakimu au jaji, na ni mla rushwa, ni haki za watanzania wangapi zilizonunuliwa kwa muda wao wa ‘neema’ waliyopewa na mheshimiwa rais?
Swali kubwa ni kwa nini uliwapa muda wa kujirekebisha? Watu ambao wamekuwa wakihujumu nchi yetu kwa miaka nenda rudi? Mheshimiwa, una kazi kubwa mbele, umewapa watanzania matumaini makubwa mno!