MWAI KIBAKI WAHURUMIE WAKENYA!
Hebu soma sura za wananchi hawa, mwangalie huyu aliyevaa shati ya bluu na anayemfuatia kulia, mwenye kapero. Unadhani wanaimaba ujumbe gani? Au wanasema nini?
Utafanya makosa kudhani kwamba haya mawe yalijipanga hapa, ni wananchi kuashiria kwamba 'enough is enough'
Kwa muda mrefu nimekuwa kimya, wengi walitarajia pia kuona nini maoni ya wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kisias kuhusu uchaguzi mkuu nchini Kenya.
Ningeweza kutoa maoni yangu mapema sana, lakini kwa kweli kilichonichelewesha ni bumbuwazi, masikitiko, huzuni na kila kinachofanana na hayo. Kinachousikitisha moyo wangu hasa si mauaji yanayoendelea nchini Kenya, bali ni kile ambacho akili yangu inaamini kuwa ni jeuri, kiburi na kutokujali kwa ndugu Mwai Kibaki.
Kibaki anajaribu kutka kuwa mmoja wa Madikteta waliowahi kuwapo Ulimwenguni. Kinachonifanya niamini haya si kwa sababu Kibaki ameshinda kiti cha urais, ushindi ambao ni tata, bali ni kitendo chake cha kukaa kimya na kuonekana kama mtu asijua kinachoendelea Kenya! Haonekani kuguswa na tatizo lililopo, na kama ni hivyo basi ni kwa maslahi ya kiti chake, kwamba kama wakenya wameweza kuzuia magari ya polisi njiani, basi kwa njia yoyote wanaweza kufanya lolote kubatilisha ushindi wake wa kizungumkuti.
Nimegusia suala la udikteta, kwa vile naamini kwamba mbali na sifa ya kutawala kibabe inayopamba udikteta, hali ya kutokujali usalama wa raia na kukosa huruma kwa wananchi ni sifa pia za udikteta.
Uchaguzi Kenya uliofanyika tarehe 27 Desemba 2007 ulianza kwa kasoro nyingi ikiwamo malalamiko kuhusu utaratibu mbovu wa orodha ya wapiga kura, kwa maelezo kwamba ilikuwa vigumu kupata majina ya waliojiandikisha. Mmoja wa wahanga wa hali hiyo ni mgombea urais wa chama cha ODM Bwana Raila Odinga.
Hata hivyo kwa wale waliokuwa wakifuatilia uchaguzi huo kwa karibu wanakumbuka kwamba kadri zoezi la uhesabuji kura lilivyoendelea ndivyo dalili za kushinda kwa Odinga zilivyoongezeka. lakini ghfla tukasikia kuwa mshindi si Odinga bali ni Kibaki ambaye kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya ECK, anaiongoza Kenya kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Tukashituka lakini tukatulia tena kwamba tume imetangaza, lakini kwa kweli waliokuwapo huko hasa wakenya wenyewe, aksema NO, wakakataa kivitendo, ghasia zikazuka, naam hata sasa watu wanakufa, polisi kwa raia nao wameuwawa.
Kinachonisikitisha mpaka sasa ni kwamba Kibaki ni Mroho wa madaraka, nasikia amekataa usuluhishi, jambo ambalo tuliliombea sana, Kibaki analazimisha kutawala wakenya waliomkataa, ndivyo inavyoonesha. Na kinachoniumiza zaidi ni kwamba sijui anajisikiaje kuona mauaji yanvyoendela huko. Kwa nini asiachie tu ngazi na ikibidi kuitisha uchaguzi mwingine kama kweli ana uchungu na Wakenya. Kwa nini askubali kufanya mazungmzo na Odinga kama kweli si Dikteta?
Anafurahia mauaji ya watu ambao wamesema inatosha kwa yeye kutawala? Kama ana uhakika na ushindi wake kinachochelewesha kuunda tume ya uchunguzi ni nini? Hata watu wa karibu wa Kibaki wamemshauri hivyo, mmoja wapo ni Mwanasheria Mkuu wa Kenya bwana Amos Wako. Inaripotiwa pia kwamba nchi wahisani wametoa dukuduku lao.
Lakini kwa mujibu wa Gazeti la Standard la Kenya, Mwai Kibaki amekataa kuwa na serikali ya Mpito na kwamba wale ambao hawajaridhishwa na matokeo ya uchaguzi huo basi wafuate sheria, anasema hivyo huku akijua kuwa pengine ni sheria hiyo hiyo ambayo yeye ameikanyaga na kutoifuata kuingia Ikulu ya Kenya. Kwa jeuri na kiburi Kibaki anasema hivi "Wale hawataki kufuata sheria tutaonana na wao" Jamani tujiulize, kama aliweza kukusanya wanasheria kumwapisha 'fasta fasta' atashindwaje kuwakusanya kudhibiti hao anaowatuma kwenye vyombo vya sheria.
Huwezi amini, yaani ninapotafakari hayo nakosa cha kusema, si kwa sababu sina, bali moyo wangu unaumia, na ndipo ninapoanza kuwafkiria viongozi wengi wa Afrika, jinsi walivyo waroho! Wasio jali watu wao na wanafiki! Wengi na sio wote!
Unaona huo ujumbe kwenye kifua cha kijana huyu? Anasema "tumechagua mabadiliko na sio mauti" Huu ni ujumbe wa umma, Umma unazungmza unasema unataka mabadiliko. Wanasiasa ni vema wakawa na busara, wananchi wakisema NO, iwe No!